Kampeni ya "VIJANA NI WAKATI WETU” Pangani kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Pangani akishirikiana na Ofisi ya Mbunge na Halmashauri imeanza rasmi kwa mwitikio na hamasa kubwa leo uwanja wa Bomani Tarafa ya Pangani mjini kama ambavyo DC Zainab Abdallah alidhamiria kukutana, kuhamasisha, kuzungumza, kutambuana na kusemezana na vijana wote wa Pangani kuwahamasisha, kuwasapoti, kuwaleta pamoja na hili likifanikiwa kwa kua na idadi yao wasio na kazi, kujua wana vipawa gani, wana malengo yapi na wanaweza kufanya nini!! (Database), kuwajua wenye elimu na wasio na elimu na ujuzi mbalimbali.
Hii imeambatana na kuwasajili, kuwagawa katika makundi kutokana na uwezo wao na malengo yao, na hatua zao; mfano mafundi ujenzi, kilimo, uvuvi, ufundi, bodaboda, washonaji, wasanii n.k.
Tumeamua kuwasapoti kuandaa mipango ya miradi, kuwapa uwezeshi wa miundombinu ikiwemo kutumia asilimia za vijana ambayo ni haki yao, kurudisha karakana zilizokufa, kuwapa sapoti kuwaunganisha na miradi ya halmashauri, ufuatialiaji na usimamizi chini ya Idara ya Vijana.
Vijana ambao wameshapiga hatua wametambuliwa na kua mfano kwa wengine ambao hawajaanza kabisa. Tukiwa viongozi vijana hatutokuwa na amani kamwe kama hatutakuwa sehemu ya kutengeneza hatma ya vijana wenzetu.
Hii ni Phase 1 ya program hii, Phase 2 itaambatana na kuwatengenezea mazingira wezeshi na mafunzo rasmi kulingana na malengo yao. Na kisha Phase 3 tutakamilisha kwa kuhakikisha hakuna kijana ambae atakaa mitaani hana shughuli maalum ya kufanya. Kampeni hii imezinduliwa na Mkuu wa Wilaya leo Tarehe 03 Sept.2018 na itahitimishwa Tarehe 06 September 2018 na itapita Tarafa zote 4 za Pangani kuanzia Pangani Mjini tarehe kuelekea Mwera Tarehe 4 septemba , Madanga tarehe 5 septemba itamalizia Mkwaja Tarehe Septemba 2018.
Uzinduzi umekua na wito kwa vijana wa Pangani kujitokeza na wamehamasika ikiwemo kujisajili rasmi. Tukutane kesho Tarafa ya Mwera - Kipumbwi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa