Kupata kibali cha ujenzi
1.Muombaji anapaswa kuwasilisha ramani ya nyumba pamoja na hatimiliki ya kiwanja ofisi za ardhi
2.Timu ya upitiaji ramani ya wilaya hukaa kwa kufuata mtiririko ufuatao ili kupitisha ramani husika
i.Afisa ardhi hukagua uhalali wa umiliki wa ardhi husika
ii.Mipango miji hukagua kama ramani husika inafuata mipango miji ya eneo husika
iii.Kitengo cha afya hukagua kama ramani husika imezingatia mifumo ya majia safi pamoja na mifumo ya maji taka ya eneo husika
iv.Mhandisi wa ujenzi huakiki michoro ya ramani kama ipo kitaalamu
3.Baada ya timu kumaliza uhakiki wanampatia muombaji hati ya kwenda kulipia kibali chake
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa