Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndg Daud Mwakabanje leo Februari 15, 2024, amewasilisha taarifa mbalimbali za Afua za Afya na Lishe zilizotekelezwa na idara mbalimbali katika kipindi cha robo ya Pili kuanzia Oktoba hadi Disemba, 2023/2024.
Aidha amehimiza kuwa ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anatekeleza Afua zote Muhimu za Lishe ikiwa ni pamoja na Mapishi ya Mfano pamoja na upimaji wa uwiano wa uzito na urefu.
Kwa upande wake ndgu Sahera Mganga ambae ni mjumbe wa kamati ya Afya na Lishe ameipongeza ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kupitia idara ya Elimu Msingi na Awali pamoja na Idara ya Elimu Sekondari kwa kuhakikisha Shule zote Wilayani Pangani zinatoa Chakula Shuleni ikiwa ni utekelezaji wa Afua za Afya na Lishe.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa