Balozi wa Mazingira na Maendeleo ndg Michael Msechu leo Tarehe 08 Novemba, 2024 amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe Gift Isaya Msuya.
Hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo ndg Michael Msechu amebainisha lengo la kutembelea Wilaya ya Pangani ni pamoja na kuhamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024 na utunzaji wa Mazingira.
Aidha kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Gift Isaya Msuya amempongeza ndg Michael Msechu kwa juhudi zake za kuhamasisha vijana kutunza mazingira na kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuongeza kuwa Wilaya ya Pangani iko tayari kwaajili ya Uchaguzi huo pamoja na kuendelea kuhakikisha mazingira yanatunzwa ipasavyo.
" Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi".
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa