Baraza la Biashara la Wilaya ya Pangani limefanya Mkutano wake wa kikatiba leo Aprili 30, 2024.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Aidha Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali wa biashara kutoka Sekta binafsi na sekta za umma ili kujadili, kupendekeza na kutatua changamoto za wafanyabiashara pamoja na mazingira ya biashara zao.
Akiongea mala baada ya ufunguzi wa mkutano huo Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bi Jenipha Nyahongo amebainisha kuwa
" Baraza la biashara ni jukwaa rasmi la majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika ngazi ya Taifa,Mkoa na Wilaya". Alisema.
Ikumbukwe kuwa, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Mussa Kilakala, aliyewakilishwa na Afisa Tarafa wa Pangani mjini bi Helswida Majula amesisitiza kuwa "-
" Changamoto mbalimbali za biashara ziangaliwe na zitatuliwe ili kuruhusu mazingira bora ya biashara".
Hata hivyo Wajumbe mbalimbali ambao ni wafanyabiashara wametoa hoja zao na lengo ni kuendelea kuboresha mazingira mazuri ya biashara katika Wilaya ya Pangani.
BARAZA LA BIASHARA LA WILAYA YA PANGANI LAFANYA MKUTANO.

Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa