Baraza la Waheshimiwa Madiwani robo ya Tatu kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2023/2024 limeketi leo tarehe 17 Mei 2024 , katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Sambamba na hilo Waheshimiwa Madiwani wamepata nafasi ya kupitia na kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli katika kipindi cha robo ya Tatu kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2023/2024.
Aidha katika kipindi cha robo ya Tatu,mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imekusanya na kupokea kiasi cha Tshs 12,967,076,092.4 ambayo ni sawa na asilimia 68 ya makisio ,Alisema Mkurugenzi Mtendaji ndugu Edward Charles Fussi
Ameongeza kuwa makusanyo ya vyanzo vya ndani pekee ni jumla ya Shilingi bilioni 1.4 sawa na asilimia 77 ya bajeti ya mapato ya ndani ya Halmashauri hadi kuishia mwezi Machi, 2024.
Vilevile Waheshimiwa Madiwani walipata fursa ya kuuliza maswali kwa TARURA, na RUASA.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa