Katibu Tawala wa Wilaya ya Pangani, Bi Ester Gama, (mwenye koti jeusi) akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Ndugu Charles Edward Fussi, wametembelea banda la Halmashauri hiyo mapema leo tarehe 2 Agosti 2025 katika viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Ziara hiyo imelenga kujionea bidhaa na teknolojia mbalimbali zinazotolewa na idara za kilimo, mifugo na uvuvi, pamoja na kuwatia moyo wataalamu na washiriki waliopo kwenye banda hilo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa mbalimbali za maendeleo kupitia sekta hizo.
Kauli mbiu " Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 20
25".
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa