Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Zainab Abdallah amefanya Ziara na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU).
Ziara hio imefanyika 22 Julai 2023 katika hospitali kongwe ya wilaya ya Pangani ambapo ujenzi huo upo katika maendeleo mazuri
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali hio Dokta Hassan Ally Msafiri amesema kuwa "mradi wa ujenzi wa chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU) unaendelea na upo hatua nzuri na mpaka sasa jumla ya shilingi milioni 250 kutoka Serikali kuu zimetumika, lakini pia tunamshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bwa Isaya M Mbenje kwa kutoa shilingi milioni 42 kutoka kwenye mapato ya ndani kusaidia ujenzi huo".
Mkuu wa Wilaya amesema kuwa "Nampongeza sana DMO na timu nzima ya hospital ya wilaya na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa kusimamia vizuri mradi huu unatekelezwa kwa awamu mbili".
#panganimpya
#hakunakilichosimama
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa