DKT SAMIA AWATIBU WANANCHI WA PANGANI
Pangani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewatibu wananchi wa Wilaya ya Pangani kwa kuwaboreshea miundombinu ya Afya katika Hospitali ya Wilaya.
Dkt Samia Suluhu Hassan amewezesha ukarabati wa hospitali hiyo kongwe kwa kuleta fedha kiasi cha shilingi milioni mia 9 na ujenzi wa jengo la wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa pamoja na kuajiri wataalamu mbalimbali katika sekta ya afya.
Hadi sasa huduma mbalimbali zinaendelea kutolewa katika hospitali hiyo.
Kwa upande wao Waheshimiwa madiwani chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri mhe Akida Bahorera wamemshukuru mhe Rais na kuahidi kuendelea kuisimamia, kuilinda miundombinu hiyo kwa vizazi endelevu.
#afyabora.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa