Tarehe 29 Mei 2025, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Pangani limewapatia wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari elimu muhimu ya tahadhari dhidi ya moto.
Mkufunzi kutoka Jeshi la Zimamoto ameendesha mafunzo hayo kwa vitendo na nadharia, yakilenga kuwaandaa vijana wetu kuwa mabalozi wa usalama majumbani na shuleni
Aidha elimu kuhusu majanga hayo ilitolewa ikiwemo Elimu ya namba ya dharura 114, Matumizi sahihi ya vizimia moto vya awali, tahadhari za kuchukua wakati wa majanga ya moto pamoja na aina zake .
Tunapongeza jitihada hizi za kuimarisha usalama na uelewa kwa wanafunzi wetu.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa