Afisa Lishe kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndg Daud Mwakabanje ameendelea kutoa elimu na kuhamasisha wanafunzi juu ya matumizi sahihi na mpangilio bora wa vyakula ili kuimarisha afya na kuepuka magonjwa yanayoweza kuwapata mara kwa mara.
Elimu hiyo imetolewa Leo tarehe 02 Februari, 2024 katika Shule ya msingi Funguni iliyopo Wilayani Pangani.
Mbali na kufundisha kuhusu mpangilio bora wa mlo kamili somo lililofundishwa na Afisa Lishe Wilaya Daud Mwakabanje, Wanafunzi pia walipata fursa ya kuuliza maswali juu ya namna bora ya kuandaa chakula bora na kupatiwa majibu na Afisa Lishe huyo.
Aidha, Afisa Lishe ameongeza kuwa suala la lishe bora linakwenda sambamba na usafi pamoja na usalama wa chakula kuanzia shambani kinapotoka mpaka muda wa kuliwa.
#Lishebora kwa kila rika
#panganimpya.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa