Halmashauri ya Wilaya ya Pangani yawakumbuka walimu wenye mahitaji maalumu kwa kuwakabidhi vitendea kazi
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imeendelea kuonesha dhamira yake katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu wenye mahitaji maalumu, baada ya kuwakabidhi vitendea kazi vitakavyowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Akikabidhi vitendea kazi hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Afisa Elimu Maalumu, Mwalimu Mathias Pori( mwenye shati jeupe), amekabidhi kompyuta mpakato mbili (2), tablet mbili (2) pamoja na vifaa saidizi maalumu kwa walimu wasioona wanaofundisha katika Shule ya Msingi Funguni.
Kwa jumla, walimu wanne (4) wamepokea msaada huo na wameishukuru Serikali pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa kuwajali na kuendelea kuboresha miundombinu na vifaa vya kujifunzia, hatua inayochangia kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu jumuishi.

Walimu hao wamesema kuwa vitendea kazi walivyokabidhiwa vitawawezesha kufundisha kwa ufanisi zaidi na kuongeza ari ya kazi, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza jitihada hizo ili kuhakikisha hakuna mwalimu au mwanafunzi anayebaki nyuma katika safari ya elimu.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa