• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Pangani District Council
Pangani District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mkakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Fedha Uchumi na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • kilimo Umwagiliaji na ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya jamii na vijana
      • Ujenzi
      • Enviroment and Sanitation
    • vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Beekeeping
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uvuvi na Hifadhi ya Bahari
    • Biashara na Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Huduma za kijamii
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmshauri
      • Kamati ya fedha ,mipango na uongozi
      • Kamati ya Elimu ,Afya na Maji
      • Kamati ya uchumi ujenzi na mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na Mh. Mwenyekiti
      • Ratiba ya vikao vya kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Repoti Mbalimbali
    • Mwongozo
    • fomu mbalimbali
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa umma
    • Hotuba
    • Video
    • Maktaba ya Picha

JINSI YA KULIPIA LESENI ZA BIASHARA

siku ya kuwekwa : August 26th, 2024

Jinsi ya Kulipia Leseni za biashara

kupata leseni y biashara hakikisha una TIN namba toka TRA


 UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA


Leseni zote za Biashara hutolewa chini ya sheria ya Biashara Na.25 ya Mwaka 1972 na Marekebisho yake yaliyofanyika june 2014 pamoja na marekebisho katika sheria ya Fedha Na.2 ya Mwaka 2014 na Na.16 ya Mwaka 2015. Mwombaji wa leseni ya biashara  anapaswa ajaze fomu ya maombi ya leseni TFN211 (Business application form).


Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane(18) Mwenye akili timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara kisheria.


Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinacho mruhusu kufanya biashara nchini kutoka idara ya uhamiaji.


LESENI ZA BIASHARA ZIMEGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI MAWILI:


KUNDI A;Leseni hizi hotelewa na Wizara ya Viwanda ,Bishara na Uwekezaji.(Fomu ya maombi iwasilishwe na Halmashauri kabla ya kupelekwa Wizarani)


Mfano;


Uagizaji bidhaa toka nje(import licence)

Kusafirisha bidhaa nje (Export licence)

Hotel za kitalii (Tourist Hotel& Lodging)

Wakala wa kupokea na kusafirisha mizigo (Clearing and Fowarding/Freight Forwarders) n.k

KUNDI B:Hizi hutolewa na Halmashauri za Wilaya,Manispaa,Miji na Majiji husika.


Mfano:


Wakala wa Bima (Insurance Agent)

Vipuri (Spare parts,Mshine tools)

Maduka ya dawa za Binadamu/Mifugo

Viwanda Vidogo (Small Scale Manufacturely and Selling)

Uuzaji Bidhaa Jumla na Rejareja (Wholesale and Retail trade) n.k

UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA


Kila Mfanyabiashara anatakiwa afike ofisi ya Biashara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa ajili ya kuchukua fomu na kujaza kama utakavyoelekezwa .Baadhi ya nyaraka zinazohitajika kama kiambatanisho na masharti katika fomu ya maombi (TFN221) ni ;


Mfanyabiashara anapaswa awe na hati ya usajili iwapo anatumia jina la biashara      ( Certificate of Registration or Incorporate).

Kama ni Kampuni mwombaji awe na memorandum and Article of Association ambazo zinaonyesha kuwa kampuni imeruhusiwa kufanya biashara anayoiomba.

Mwombaji awe na umri wa miaka 18 au zaidi

Awe na mahali/Eneo linalokubalika kwa aina ya biashara anayoiomba  na isiwe vidanda vilivyopo kando kando ya barabara.

Awe na TIN certificate.

Awe na hati ya kuthibitisha uraia wake kama,Nakala ya Hati ya Kusafirisha”passport”ya Tanzania,cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo(Affidavit) au Kitambulisho cha Mpiga kura.Kama ni mgeni awe na hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Resident Permit Class “A”.)

Masharti mengine ya kupata leseni hutegemea aina ya biashara mtu anayetaka kuanzisha  e.g. Mgahawa,Dawa za Binadamu na Mifugo,Vyakula,Nyama na Samaki inabidi afuate taratibu zote za afya na kupima wafanyakazi wake

Hati ya Utaalam (Professional Certificates) kwa biashara zote za kitaalam

Maombi mapya yatapitia ngazi za Serikali ya Mtaa/kijiji ,Afya na Kisha ofisi ya biashara kwa ajili ya utoaji wa leseni.

MALIPO:Kutokana na marekebisho ya sheria ya fedha Na 2 ya mwaka 2014 ada za leseni hulipwa kulingana na aina ya biashara kama ilivyoanishwa katika jedwali la viwango vya ada kwa mwaka


MUDA WA LESENI: Umri wa leseni ni miezi 12 toka siku ya kutolewa.




MASHARTI YA UTUMIAJI WA LESENI


1.Mwenye leseni hataweka masharti yeyote kwa mnunuzi


2. Mwenye leseni atatoa risiti kwa mauzo yote.


3.Mwenye leseni atafuata sheria ya leseni ya biashara No. 25 ya 1972


4.Mwenye leseni hatatoa huduma/bidhaa ambazo hazizingatii viwango vya ubora,uliowekwa na Vyombo vinavyotumika kisheria


5.Mwenye leseni anaweza kunyang’anywa wakati wowote ikiwa inaonekana aliipata kwa njia ya udanganyifu au amekiuka masharti ya leseni.


MAKOSA


   1.Kuendesha biashara bila leseni


   2.Kuendesha biashara eneo tofauti na linaloonyeshwa kwenye Leseni.


  3.Kutumia leseni moja kufanya biashara zaidi ya moja au maeneo mawili au zaidi


  4.Kushindwa kuonyesha leseni ya biashara inapotakiwa kufanya hivyo na Afisa aliyedhinishwa na Serikali.


  5.Kutokuweka leseni ya biashara mahali ambapo inaonekana kwa urahisi (Kuficha leseni).


  6.Kutoa maelezo ya uongo ili kupata leseni au kukwepa kulipa ada /kodi inayostahili


  7.Kumzuia Afisa wa Serikali aliyepewa mamlaka ya kukagua kufanya kazi yake.


ADHABU;  (i). Mtu yeyote anayetenda mojawapo ya makosa hapo juu adhabu yake ni faini isiyopungua Tsh 50,000/= na isiyozidi Tsh 100,000/= au kifungo kisichozidi miaka miwili(2) au faini na kifungo kwa pamoja.


                  (ii). Mtu yeyote atakayechelewa kuhuisha leseni yake baada ya siku 21 baada ya     muda wa leseni kuisha atalipia asilimia 25 ya ada iliyotakiwa kulipia na itaongezeka asilimia 2 kila mwezi kadri mfanyabiashara anavyochelewa kuhuisha leseni ya biashara


NB.Wafanyabiashara wote wanaaswa kufuata na kutekeleza sheria bila shuruti,kwani kutofanya hivyo kunawaingiza gharama zisizo za lazima kama faini na kupoteza muda hasa pale wanapokutwa na makosa

Tangazo

  • MPYA: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI May 10, 2023
  • MPYA: TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • MPYA: ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUENDELEA NA USAILI WA MAHOJIANO September 09, 2023
  • MPYA: ORODHA YA WATAKAOENDELEA NA USAILI WA MAHOJIANO September 09, 2023
  • Angalia zote

Habari za Sasa

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI.

    May 23, 2025
  • WILAYA YA PANGANI YAFANYA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE – ROBO YA TATU 2024/2025.

    May 19, 2025
  • RC BATILDA AIPONGEZA PANGANI UANDIKISHAJI WA DAFTARI AWAMU YA KWANZA NA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUJITOKEZA AWAMU YA PILI

    May 16, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI NA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI LAANZA PANGANI

    May 16, 2025
  • Angalia zote

Video

ujenzi wa barabara ya Tanga pangani
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Mwongozo wa Tehama
  • Ratiba ya Vikao vya Halmashauri
  • Miongozo mbalimbali

Kurasa za mfanano

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Miongozo mbali mbali
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Pangani District Council

    Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga

    Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058

    Namba ya simu: 0658100588/062289307

    Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz

Mawasiliano Mengineyo

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa