KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA YA FEDHA, MAPATO PAMOJA NA MATUMIZI.
Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, imefanya kikao cha kupokea na kujadili taarifa ya Fedha,Mapato na Matumizi kwa mwezi Oktoba 2023.
Kikao hicho kimefanyika Novemba 28, 2023 katika ukumbi wa Zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Kamati imepokea na kujadili taarifa mbalimbali kama vile Mapato na Matumizi,pamoja na Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri mhe Akida Bahorera, ambae pia ni Diwani wa kata ya Kipumbwi, ametoa rai kwa Wataalamu kuendelea kushikamana na kusimamia Miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ili kuijenga Pangani bora.
Mhe Bahorera ameipongeza Halmashauri kwa kuendelea kujituma katika suala zima la ukusanyaji wa Mapato na kuwaomba wazidi kuongeza nguvu ili kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa wakati na kuzingatia sheria.
Kikao hiki kinafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa ya Mwaka 2009 agizo namba 21.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa