Wakazi wa Kijiji cha Buyuni wilayani Pangani wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha huduma za afya kupitia ujenzi wa zahanati mpya kijijini hapo.

Shukrani hizo zimetolewa leo, tarehe 7 Januari 2026, wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa zahanati hiyo iliyoongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Ndugu Agape Fue.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Buyuni ndugu Diwani Akida amesema tangu kuanzishwa kwa kijiji hicho hakujawahi kuwa na zahanati, na hivyo wananchi wamekuwa wakilazimika kutembea zaidi ya kilometa 20 kufuata huduma za afya.

Amesema:“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutuwezesha kupata zahanati hii. Kweli Buyuni tumefarijika sana.” Alisema
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Agape Fue amewataka wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ili wananchi waanze kupata huduma mapema, akibainisha kuwa hata fedha za vifaa tiba tayari Serikali imekwishatoa.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa