Tarehe 31 Januari 2024 Kijiji cha Msaraza kata ya Bushiri Wilayani Pangani kimefanya maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe.
Zoezi hilo lenye lengo la kutekeleza Mkataba wa Lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani limeendelea kutekelezeka kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kutekeleza afua mbalimbali za Lishe.
Miongoni mwa Afua muhimu zinazotekelezwa ni pamoja na maadhimisho ya Siku ya afya na Lishe(SALiKi) yanayofanyika kila robo kwa kila kijiji.
Jumla ya Wananchi 56 ( 16 me na 40 ke) wamehudhuria na kupatiwa Elimu ya Lishe, Kupima Uzito kwa watoto , kupima kipimo cha Muac kujua hali ya Lishe kwa watoto na Elimu nyingine jumuishi.
Jumla ya watoto 53 (29 ke na 24 me) wamepimwa hali zao za lishe kutumia kipimo cha muac na hali zao wote ziko vizuri(wote kipimo kimeonyesha alama ya kijani), hivyo hakuna mtoto mwenye utapiamlo.
Pamoja na hayo huduma zingine zimetolewa ikiwemo kutoa kufanya mapishi ya mfano.
#panganimpya
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa