Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imefanya kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza leo Alhamisi Oktoba 26, 2023, kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo baraza limepokea taarifa za utekelezaji wa kazi katika ngazi ya Halmashauri kwa kipindi cha robo ya kwanza.
Kikao kimefanyika kwenye ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali ikiwa ni kikao cha wazi.
Akipokea taarifa za utekelezaji wa kazi kutoka kamati mbalimbali za Halmashauri. Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Akida Bahorera amewashukuru waheshimiwa madiwani na wataalamu pamoja na taasisi mbalimbali kwa kufanikiwa kupokea taarifa za utekelezaji wa kazi.
“Kwanza niwashukuru Waheshimiwa madiwani kwa kuweza kufanya kikao hiki cha baraza salama na kupokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Hata hivyo Mwenyekiti amemshukuru Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan,kwa miradi ya maendeleo,pamoja na mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Zainab Abdallah na Mbunge ambae pia ni Waziri wa maji mhe Jumaa Aweso kwa kuendelea kuisemea vema Wilaya ya Pangani.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa