Pangani -Tanga
Mkurugenzi msaidizi Idara ya jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum bi Juliana Kibonde, ameshiki Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili kupitia kampeni ya kuelekea miaka 30 ya Beijing, yenye kauli mbiu ya " Chagua kutokomeza ukatili wa kijinsia, ambapo amesema ni jukumu la Jamii nzima kutoa taarifa za kupinga ukatili wa kijinsia.
Ameyasema hayo leo tarehe 6 Desemba, 2024, alipokua katika mwendelezo wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Wilayani Pangani.
Nae Mhe,Heliswida Simon Majula mwakilishi kutoka Ofisi ya mkuu wa wilaya ya pangani amesema kuwa
" kila mmoja katika Jamii yetu ana haki ya kukataza vitendo viovu vya ukatili ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia". Alisema.
Sambamba na hayo Balozi wa Ireland bi,Hellen amesema anaishukuru Serikali pamoja na wadau mbalimbali wanao pinga ukatili wa kijinsia kwa kuweka mazingira sawa katika kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Kwa upande mwingine viongozi wa dini zote wamekemea vikali vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia Kwa wanawake na kuwataka wazazi kuwaangalia vyema watoto wao.
Maadhimisho hayo ya Sikua 16 za Kupinga Ukatili, yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, pamoja na Taasisi mbalimbali zikiwemo UZIKWASA, Easun, Femina hip, ESTL,WOLEA, TARIRI, AMREF, CAN Tanzania, ambazo kwa pamoja zinapinga maswala haya ya ukatili wa kijinsia kwa ujumla.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa