Leo tarehe 5 Disemba 2025, Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wameapishwa rasmi katika ukumbi wa mikutano wa YMCA – Pangani.

Tukio hili muhimu limefungua ukurasa mpya wa uongozi na utumishi kwa wananchi wa Pangani.
Aidha katika shughuli hiyo, zoezi la uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri limefanyika ambapo Waheshimiwa Madiwani wamemchagua kwa kura za kishindo Mhe. Sefu Ally Said (Mapepo) diwani wa kata ya Ubangaa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Mhe Zainab Mvaa diwani wa viti maalum kuwa Makamu Mwenyekiti katika kipindi cha 2025–2030.
Baada ya kutangazwa mshindi, Mhe. Sefu Ally Said ametoa shukrani za dhati kwa waheshimiwa madiwani wote kwa imani waliyoonyesha kwake, huku akiahidi Uongozi wenye weledi na uwajibikaji na Ushirikiano mzuri na viongozi pamoja na watumishi wote wa Serikali.

Ameongeza kuwa ataendelea kusimamia miradi mbalimbali kwa maendeleo chanya ya wananchi w
a Pangani.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa