Asante Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Maendeleo makubwa uliyoyafanya Wilayani Pangani kwa kipindi cha miaka mitatu ( 3) ya uongozi wako.
Pangani inashukuru kwa uboreshaji wa huduma za Usafirishaji ikiwemo ujenzi wa Daraja la kihistoria Wilayani Pangani lenye urefu wa Mita 525.
Aidha ujenzi wa daraja hili litaunganisha barabara ya Tanga_ Pangani hadi Bagamoyo mkoani Pwani kupitia Saadani ambapo jumla ya Shilingi Bilioni 82.19 zimetengwa kukamilisha mradi huu.
Aidha Pangani inamshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya balabala, ikumbukwe kuwa ujenzi wa Daraja hili lina kwenda sambamba na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tanga_Pangani (km 50) na tayari wakandarasi wanaendelea na miradi hii mikubwa.
Pangani inaendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa vitendo.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa