Mamlaka ya bandari Tanzania imekabidhi msaada wa vifaa tiba vya kutolea huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya pangani, tarehe 13/06/2023.
Vifaa hivyo ni Pamoja na, Magodoro kumi na tano (15) kwa ajili ya matumizi ya wodini, vitanda kumi na tano (15) kwa ajili ya matumizi ya wodini, kabati ndogo (Bed side locker metal) kumi na mbili. Vifaa hivyo vina jumla ya thamani ya shilingi milioni thelasini na moja laki tisa tisini na nane elfu mia saba na nane tu (31,998,708/=).
Meneja wa Bandari Tanga, Bw Masoud Mrisha. Kwa Niaba ya Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, alisema “ Pamoja na kwamba Halmashauri ya wilaya Pangani ina vituo vya Afya na Zahanati nyingi za kutolea huduma za Afya, lakini tutajitaidi kadiri iwezekanavyo ili vifaa hivi viweze kugusa maeneo mbalimbali ya utoaji wa huduma za Afya na vitaisaidia Halmashauri ya Wilaya Pangani hasa katika uboreshaji wa utoaji wa huduma hasa kulaza wagonjwa”
Vile vile Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Pangani Bw Isaya M. Mbenje alisema “natoa shukurani za dhati kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuipatia Halmashauri ya wilaya ya Pangani vifaa tiba kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za Afya, Mungu awabariki sana na siku nyingine waweze kuikumbuka Halmashauri ya wilaya ya Pangani ili kuendelea kuboresha na kuongeza upatikanaji wa vifaa tiba katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Shukurani za pekee ziende kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapatia ruhusa ya kuifikia Halmashauri ya Wilaya Pangani.”
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa