Asante Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Maendeleo makubwa uliyoyafanya Wilayani Pangani kwa kipindi cha miaka mitatu ( 3) ya uongozi wako.
Pangani inashukuru kwa uboreshaji wa huduma za afya ikiwemo ujenzi wa jengo jipya kwaajili ya huduma kwa wagonjwa mahututi (ICU), pamoja na ununuzi wa Vifaa tiba, ambapo jumla ya Shilingi milioni 500 zimetumika katika ujenzi wa mradi na ununuzi wa hivyo vifaa muhimu.
Aidha Pangani inamshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuajiri Watumishi wa kada mbalimbali za Afya kwa lengo la utoaji huduma bora kwa wananchi.
Pangani inaendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa vitendo , kwa kuhakikisha inalinda Rasilimali hizo za majengo,vifaa tiba na kutoa huduma bora kwa wananchi wote.
#miakamitatu ya mama
#panganimpya
#hakunakilichosimama
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa