Mkutano wa Baraza la Madiwani umefanyika leo Julai 28,2023 katika Ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya.
Mkutano umeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Ndg, AKIDA OMARI BAHORERA,na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw. ISAYA M MBENJE.
Waheshimiwa Madiwani wa kata zote 14,walihudhuria , Katibu Tawala Wilaya, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo, Maafisa Tarafa, Watumishi,Viongozi wa Dini pamoja na Wananchi wa Pangani.
Katika Mkutano huo masuala mbalimbali ya Maendeleo yalipata nafasi ya kujadiliwa ikiwa ni pamoja na Taarifa ya Mapato na Matumizi na Miradi ya maendeleo ya Halmashauri, Hata hivyo taarifa zote zilizowasilishwa zilipokelewa.
Kamati zilizowasilisha taarifa za robo ya nne Aprili hadi Juni,2023, ni pamoja na,Kamati ya Fedha,Mipango na Uongozi,Elimu na Afya,Uchumi,Ujenzi na Mazingira, na Kamati ya Kudhibiti UKIMWI.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa