"Wilaya imeendelea kutoa Elimu na huduma ya Upimaji bure ya virusi vya Ukimwi hizi ni jitihada za kupambana na maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi." katika kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani, sisi kama Wataalam tunaendelea kutoa ushauri kwa jamii zetu kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari vilivyopo Wilayani Pangani".
Hayo yamesemwa leo Disemba 1, 2023 na Mratibu wa Ukimwi dkt Anold Mtanzi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika katika Ofisi ya Mtendaji Pangani Magharibi.
Wananchi mbalimbali wamejitokeza kupima na kujua afya zao na wameendelea kutoa wito kwa jamii kuendelea kujikinga na kukinga na wengine dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
Jumla ya vituo 23 Wilayani Pangani vinatoa huduma ya kupima bure Afya na kutoa ushauri na tiba bure.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Jamii iongoze kutokomeza UKIMWI".
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa