Shule Mpya ya Sekondari Muhembo sasa imekamilika kwa asilimia 100!
Mradi huu umegharimu Shilingi Milioni 584.28 kutoka Serikali Kuu, na sasa wanafunzi wa eneo hili hawatatembea tena umbali mrefu kufuata elimu ya sekondari.
Miundombinu ya kisasa imejengwa, ikiwa ni pamoja na madarasa, maabara, mabweni, na ofisi za walimu — yote yakiwa tayari kwa matumizi.
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani inamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika elimu na mazingira bora ya kujifunzia.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa