Pangani, Tanga
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba ya wakuu wa idara, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuboresha makazi ya watumishi wa umma na kuongeza ufanisi wa kiutendaji.
Mpaka sasa, ujenzi huo unaendelea kwa kasi na umefikia hatua nzuri, ukiashiria dhamira ya Serikali katika kuimarisha huduma kwa wananchi kupitia mazingira bora ya kazi kwa watumishi wake.
Akizungumza kuhusu maendeleo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndg Charles Edward Fussi amesema kuwa " Mradi huu ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapata huduma muhimu zikiwemo makazi bora karibu na maeneo yao ya kazi".
Aidha nyumba hizo zitasaidia kupunguza changamoto ya makazi kwa watendaji na hivyo kuongeza ari ya kazi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa