UZINDUZI WA KAMPENI YA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imedhamiria kuendeleza mikakati dhabiti ya kuwakinga wananchi na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Hayo yamesemwa leo tarehe 07/02/2025 katika kikao cha kimkakati cha umezeshaji dawa kinga za Minyoo Tumbo,Kichocho na Matende na Mabusha[Ngirimaji] kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe Gift Msuya kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTD) Wilaya ya Pangani, Dkt. Jumanne Akilimali, alianza kwa kubainisha magonjwa hayo ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele wilaya ya Pangani ambayo ni pamoja na Kichocho,Minyoo Tumbo na Matende na Mabusha [Ngirimaji].
Pia,Dkt.Akilimali ameongeza kuwa, ili kukabiliana na tatizo hilo Idara ya Afya Pangani kwa kushirikiana na wizara ya Afya itaendesha zoezi la utoaji wa Dawa kingatiba kwa watoto wa umri kuanzia miaka 5 hadi miaka 14 wa shule zote ambapo zoezi hilo litaanza siku ya tarehe 17-18/02/2025 na kingatiba ya Matende na Mabusha [Ngirimaji] kuanzia Tarehe 21-28/02/2025 kwa wanachi wote wenye miaka 5 na kuendelea.
Aidha,aliongeza kuwa zoezi hilo litasimamiwa na walimu wakishirikiana na watumishi wa Afya na lengo ni kuwafikia wanafunzi pamoja na wananchi wote kiujumla.Hii itasaidia kuondokana na changamoto za zilizokithiri za udumavu, utapiamlo na upungufu wa damu kwa watoto na uwepo wa matende na Mabusha [Ngirimaji] kwa watu wazima.
Wizara ya Afya kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele imekua ikiiendesha mazoezi haya kwa miaka sasa ili kutokomeza matatizo haya sugu katika jamii ya Pangani hivyo kila mwananchi anaaswa kushiriki kumeza dawa kinga ili kutokomeza Kichocho,Matende na Mabusha[Ngirimaji]
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa