Wakandarasi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamewasili wilayani Pangani kwa ajili ya kukamilisha zoezi la kusambaza umeme katika vitongoji vyote vilivyosalia.

Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa wananchi wote wa maeneo hayo wanapata huduma ya umeme, hatua itakayochochea maendeleo ya kiuchumi na kuboresha huduma za kijamii.
Wananchi wameeleza matumaini makubwa kuwa mradi huu utaongeza fursa za biashara, kuboresha elimu na huduma za afya, pamoja na kuinua kiwango cha maisha kwa ujumla.
Ukumbuke kuwa hadi sasa tayari Vijiji vyote Pangani vimepatiwa huduma ya Umeme.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa