Wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wameishukuru serikali kwa kuwawezesha na kuwasaidia kuinua kipato cha kaya kupitia mradi huo.
Wametoa pongezi hizo mbele ya Mratibu wa TASAF Wilaya ya Pangani bi Asnath Mtei leo tarehe 29 Januari 2025 alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Choo cha Stendi Kwakibuyu kilichojengwa kupitia mradi wa TASAF kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Wakizungumza kuhusiana na mafanikio waliyopata, baadhi ya wanufaika hao wamesema awali walikuwa wakiishi maisha duni lakini baada ya kuja mpango huo wa TASAF wa kuwezesha kaya za walengwa kwasasa maisha yao yanaendelea kuneemeka.
Wanufaika walieleza kuwa kupitia TASAF, waliweza kupata ajira za muda, ujuzi mbalimbali kipindi cha utekelezaji wa mradi, wameweza kusomesha watoto na kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo, na sasa wanajivunia mafanikio waliyopata. Vile vile kijiji kimeweza kupata miundo mbinu ya kudumu kwa marndeleo ya kijiji kwa ujumla.
Akiongea mara baada ya kutembelea mradi huo Bi Asnath amesema kuwa mradi wa ujenzi wa Choo cha Stendi Kwakibuyu ni moja ya mikakati ya kuboresha miundombinu ya kijamii.
Bi Asnath amewataka wanufaika kuendelea kutunza miundombinu iliyopatikana kutokana na mpango wa TASAF kwa namna bora ili kupata manufaa zaidi na kuendeleza maendeleo ya jamii zao.
Pia ameishukuru serikali chini ya uongozi wa Rais Samia kuendelea kuona umuhimu wa kuziwezesha kaya za walengwa kwani bado baadhi ya kaya zinauhitaji wa kuendelea kunufaika
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa