Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wameanza kupatiwa Mafunzo ya Mfumo wa Upimaji Utendaji kazi kwa watumishi wa Umma (PEPMIS).
Mafunzo hayo yameanza leo tarehe 6,Disemba 2023 hadi 7, Disemba 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Pangani, yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, yakiwahusisha Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri na wasaidizi wao.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu ndg Veronica Marwa.
Amesema kuwa mfumo huo, utawezesha upimaji wa kazi alizopangiwa mtumishi kwa siku, kulingana na majukumu aliyopangiwa na muda wa kufikia malengo pamoja na tathmini na upimaji.
Naye mtoa mada kutoka Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, ndg Kamugisha Sabas amesema, mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi, yenye lengo la kumuwezesha mtumishi wa Umma, kujifanyia upimaji wa kazi anazozitekeleza kila siku kupitia mfumo wa PEPIMS.
"Kila mtumishi anapaswa kuuelewa vizuri mfumo huu, kwa kuwa unamgusa moja kwa moja utendaji wake wa kazi, kwa kuzingatia malengo binafsi na kufikia malengo ya jumla ya Mwajiri ambaye ni Serikali, niwasisitize nafasi hii ni muhimu kwa kila mtumishi, kuhakikisha unauelewa vizuri mfumo huu mpya wa PEPMIS" .
Amebainisha kuwa, lengo la mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo watumishi na kuwa na uelewa wa pamoja wa namna ya kutumia mfumo wa PEPIMS, ambao ni mfumo mpya uliotolewa na serikali kwa ajili ya kupima utendaji kazi kwa watumishi wote wa Umma.
#panganimpya
#kaziiendelee.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa