Mhe. Prof. Makame Mbarawa,Waziri wa ujenzi na uchukuzi, amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa daraja la muda la mto Pangani, Agosti 28,2023.
Prof. Makame ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe Zainab Abdallah, Waziri wa Maji (mb) wa jimbo la Pangani mhe Jumaa Aweso,Mwenyekiti wa Ccm Mkoa Mh. Rajabu Abdurrahman,Mwenyeketi wa Halmashauri Mhe Akida Bahorera na viongozi mbalimbali wa CCM.
Prof. Makame amepongeza juhudi za ujenzi wa daraja hilo la muda, ambalo limekamilika kwa 100% na tayari kwa kuanza ujenzi wa daraja la kudumu.
"Niwaombe wakandarasi wajenge daraja lenye ubora na viwango vya juu,ili liweze kutoa huduma yenye tija kwa Taifa letu la Tanzania".
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Zainab Abdallah, amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha za ujenzi wa Daraja la mto Pangani,ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Pangani kwa ujumla.
Daraja la mto Pangani linatarajiwa kukamilika Disemba,2025 kwa mujibu wa mkataba.
#panganimpya
#kaziiendelee
#hakunakilichosimama.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa