• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Pangani District Council
Pangani District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mkakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Fedha Uchumi na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • kilimo Umwagiliaji na ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya jamii na vijana
      • Ujenzi
      • Enviroment and Sanitation
    • vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Beekeeping
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uvuvi na Hifadhi ya Bahari
    • Biashara na Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Huduma za kijamii
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmshauri
      • Kamati ya fedha ,mipango na uongozi
      • Kamati ya Elimu ,Afya na Maji
      • Kamati ya uchumi ujenzi na mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na Mh. Mwenyekiti
      • Ratiba ya vikao vya kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Repoti Mbalimbali
    • Mwongozo
    • fomu mbalimbali
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa umma
    • Hotuba
    • Video
    • Maktaba ya Picha

WILAYA YA PANGANI YAFANYA UZINDUZI WA VITABU VYA MKAKATI WA KUONGEZA UFAULU KWA NGAZI YA ELIMU MSINGI NA SEKONDARI

siku ya kuwekwa : September 16th, 2022

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa sera ya Elimumsingi Bila Malipo. Pia, kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023 wanafunzi wa kidato cha Tano na sita hawatalipa ada. Lengo ni kuhakikisha  kuwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapata nafasi hiyo na kukamilisha mzunguko wa Elimu ya Msingi na Sekondari bila vikwazo

Pamoja na mafanikio haya, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imebaini kuwa, uendeshaji wa elimu una changamoto ambazo hazina budi kutatuliwa ili kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu. Kwa kuzingatia hilo, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeandaa mkakati wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya elimumsingi na pia changamoto za uboreshaji wa Elimumsingi na Sekondari, nini Kifanyike.

Mkakati huu umebainisha changamoto mbalimbali zinazoathiri ufanisi na mafanikio katika elimu. Aidha , mkakati umechambua kwa undani hali halisi ilivyo na kuonesha fursa zilizopo, utatuzi wa changamoto pamoja na viashiria vya upimaji wa mafanikio ya utekelezaji wa mkakati huo.

Mkakati huu ni zana muhimu itakayoisaidia Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji na hivyo kuwa na wahitimu wenye umahiri uliokusudiwa

Uzinduzi wa mkakati ulifanyika kitaifa Mkoani Tabora na Baadae kufanyika ki mkoa, Wilaya, Halmashauri,Tarafa, Kata, Mtaa/kijiji na kila shule. Hivyo Kila kiongozi ataweka utaratibu unaoendana na mazingira ya eneo lake ili kuhakikisha kua mkakati huu unatekelezwa na kuleta matokeo tarajiwa. Kila mdau anayehusika na utekelezaji wa mkakati huu autumie kama kioo cha kujipima ni kwa namna gani wajibu na majukumu yake

Ili kutekeleza hilo, Wilaya ya Pangani imefanya uzinduzi wa mkakati ki Wilaya, uzinduzi huo umefanyika  Leo tarehe 16/09/2022  saa 8:00 asubuhi katika Ukumbi wa Seaside. Uzinduzi huo ulihudhuliwa na Mwanyekiti wa Uzinduzi huo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mh.Ghaibu Lingo pia Uzinduzi huo ulihudhuliwa na DAS wa Wilaya ya Pangani, Hassani Nyange,  Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Lucy Gurtu ambaye ni Afisa elimu sekondari Wilaya ya Pangani, Kaimu Afisa elimu Sekondari na pia Kaimu Afisa Elimu Msingi Bw Leonard Komba, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi Wilaya ya Pangani, katika uzinduzi huo pia walikuwepo Wah. Madiwani wote wa Kata mbalimbali za Wilaya ya Pangani, Wakuu mbalimbali wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Maafisa Elimu Kata wa kata zote za Wilaya ya Pangani, Viongozi mbalimbali wa Dini, Wadau mbalimbali wa Elimu na Walimu Wakuu wa Shule za msingi na sekondari Wilaya ya Pangani

Tangazo

  • MPYA: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI May 10, 2023
  • MPYA: TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • MPYA: ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUENDELEA NA USAILI WA MAHOJIANO September 09, 2023
  • MPYA: ORODHA YA WATAKAOENDELEA NA USAILI WA MAHOJIANO September 09, 2023
  • Angalia zote

Habari za Sasa

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI.

    May 23, 2025
  • WILAYA YA PANGANI YAFANYA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE – ROBO YA TATU 2024/2025.

    May 19, 2025
  • RC BATILDA AIPONGEZA PANGANI UANDIKISHAJI WA DAFTARI AWAMU YA KWANZA NA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUJITOKEZA AWAMU YA PILI

    May 16, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI NA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI LAANZA PANGANI

    May 16, 2025
  • Angalia zote

Video

ujenzi wa barabara ya Tanga pangani
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Mwongozo wa Tehama
  • Ratiba ya Vikao vya Halmashauri
  • Miongozo mbalimbali

Kurasa za mfanano

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Miongozo mbali mbali
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Pangani District Council

    Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga

    Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058

    Namba ya simu: 0658100588/062289307

    Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz

Mawasiliano Mengineyo

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa