UTANGULIZI
Wilaya iinatekeleza shughuli zote za Uvuvi kama ilivyo ada, shughuli hizo ni pamoja na kusimsmia sheria, kanuni na sera za uvuvi ili kuhakikisha kunakuwepo na ulinzi,uhifadhi,utunzaji na uvunaji endelevuwa rasilimali za uvuvi pamoja na utunzaji wa mazingira yake,lengo kuu ni kuhakikisha rasilimali ya uvuvi inatumiwa na kizazi cha sasa na cha baadae kwa maendeleo ya jamii na wilaya kwa ujumla.
HALI YA UVUVI
Hali ya uvuvi katika wilaya yetu ya pangani ni ya wastani pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo za uvuvi haramu zana duni na vyombo duni kwa wavuvi wengi wa pangani lakini shughuli za uvuvi zimeendelea kufanyika hadi kufikia robo ya pili ya mwaka2016/2017 jumla ya kilo 38,525 zenye thamani ya tshs 154,100,000/= zilivunwa.
HUDUMA ZA UGANI
Huduma za ugani zinazotolewa ni pamoja na ufugaji samaki, ukulima wa mwani,uvuvi unaozingatia uhifadhi wa mazingira pamoja na uundaji wa vikundi vya usimamizi shirikishi wa rasilimali za uvuvi yaani Beach Management Unit(BMUs) na kuvijengea uwezo wa kufanya kazi ikiwa ni pamoja na mafunzo.
IDADI YA WAVUVI NA VYOMBO
Kwa mujibu wa sense ya uvuvi iliyofanyika mwezi wa pili mwaka 2016 Wilaya ya Pangani ina jumla ya wavuvi1540 wanaojishughulisha na uvuvi wa samaki, pweza kamba na kaa na wavuvi 62 wanaojighulisha na utandaji wa uduvi ambao kwa mujibu wa sheria ya uvuvi no.22 ya mwaka 2003.
Mchanganuo vyombo 271 vya uvuvi
s/n
|
Aina ya chombo
|
Idadi
|
1
|
Ngalawa
|
196
|
2
|
Madau
|
2
|
3
|
Boti
|
9
|
4
|
Mashua
|
13
|
5
|
Mitumbwi
|
51
|
|
Jumla
|
271
|
MAFANIKIO
Kitengo cha uvuvi kwa kushirikiana na mamlaka ya chuo cha ufundi stadi VETA kwa awamu tofauti tulifanikiwa kutoa elimu kwa wavuvi sitini (60) juu ya ujasiriamali, uchakataji na usindikaji wa samaki, VVU na Ukimwi kwa wadau wa uvuvi wa vijiji vya Ushongo, Stahabu, Pangani mashariki na Pangani magharibi na (wavuvi kumi na tano kwa kila kijiji) kuweza kutunukiwa vyeti kwa wavuvi hao. Sambamba na mtaalamu mmoja wa uvuvi aliefanikiwa kwenda kujiendeleza kwa ngazi ya shahada.
Mbali na wavuvi hao kupata elimu bado wavuvi wameendelea kupata kipato kutoka katika sekta ya uvuvi kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za uvuvi na kufanikiwa kuvuna tani 65,079 zenye thamani ya Tshs 182,316,000 /= kwa mwaka 2015/2016 ukilinganisha na tani 52,506 zenye thamani ya Tshs 151,105,880/= waliovunwa kwa mwaka 2014/2015.
Kitengo cha uvuvi kimefanikiwa katika suala zima la ukusanyaji maduhuri ambapo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 kitengo cha uvuvi kiklipangiwa kukusanya Tshs 32,598,400/= na kuweza kuvuka lengo kwa kukusanya Tshs 35,517290/= sawa na asilimia miamoja ishirini na moja (121%) ukilinganisha na mwaka 2014/2015 ambapo lengo lilikua Tshs 27,598,400/= na kufanikiwa kukusanya Tshs 23,889,650/= sawa na asilimia sabini na tatu(73%)
AINA YA SAMAKI WANAOPATIKANA PANGANI.
CHANGAMOTO
Kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta uvuvi katika wilaya Pangani changamoto hizo zimegawanywa kwa makundi yafuatayo:-
Kwa wavuvi- Changamoto kubwa walionayo wavuvi wa pangani ni zana na vyombo vyao kuwa duni hivyo kupelekea wavuvi wengi kufanya uvuvi mdogo na unaogharimu muda mwingi na mavuvi kidogo hivyo kupelekea kuwa na kipato kidogo.
Uvuvi haramu
Uvuvi haramu bado ni changamoto mbali na kitenggo cha uvuvi kujitahidi kufanya doria za mara kwa mara .
Kitengo cha uvuvi kimefanya jumla ya doria tisa (9) kuanzia mwaka 2015 mpaka sasa na kufanikiwa kukamata zana haramu ambazo ni kokoro/juya ishirini na moja(21),Nyavu za timba(monofilament) kumi na tano(15).Nyavu za makila zenye matundu madogo(gillnet) tano (5),Vimia (castnet) kumi na tano(15) na mikuki/michinji ishirini na sita (26) na kamba zenye urefu wa mita 9,400.
Sambamba na doria hiyo watuhumiwa ishirini na nne(24) walikamatwa na kupigwa faini na wengine wawili(2) kufikishwa polisi kutokana na uzito wa makosa yao na kufunguliwa kesi zenye jalada DOGORI NA SUFIANI - PAN/218/2017 (uvuvi wa sumu eneo la Mkwaja) wavuvi wengine walikimbia na kutelekeza pikipiki mbili ambazo zipo kituo cha polisi huku wakitafutwa kwa hati ya kukamata namba PAN/RB/36/2017 na PAN/RB/163/2017
Changamoto ya ukosefu wa Ruzuku ya uendeshaji wa ofisi (OC)
Kitengo cha uvuvi kimekua na changamoto nyingi ya uwezeshwaji ili kutekeleza majukumu yake ambapo imekukuwa ikitegemea mapato ya ndani kwa kuwa haipati ruzuku kutoka serikali kuu. Pamoja na kuchangia mapato mengi katika Halmashauri kitengo cha uvuvi hakirejeshewi asilimia 15 ya makusanyo kama ilivyoelekezwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kutokana na Halmashauri kuwa na vyanzo vichache vya mapato ambavyo havikidhi mahitaji ya fedha ya Halmashauri
Ukosefu wa Vitendea kazi
Aidha kitengo cha uvuvi kimekuwa na uhaba wa vitendea kazi kama vile boti ya doria kwa ajili ya kufanya doria za majini, kwa sasa Boti ndogo iliyoletwa chini ya Mradi wa MACEMP ndiyo inayosaidia doria ndogondogo kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa kufanya doria
1 MATARAJIO NA UTATUZI WA CHANGAMOTO
Matarajio ya kitengo cha uvuvi ni kuendelea kupambana na kuhakikisha tunadhibiti utoroshaji wa mazao ya uvuvi ili kuweza kufikia lengo la kukusanya Tsh 150,000,000/= ambapo hadi kufikia tarehe ishirini ya mwezi wa pili (28/02/2017) tulikua tumeshakusanya Tshs 75,000,000/= ni matarajio yetu kuwa ikiwa asilimia 15 ya makusanyo haya yatarudishwa kwenye kulinda kutunza na kuhifadhi rasilimali ya uvuvi tutafikia lengo la kuongeza mazao ya uvuvi kufikia tani 80,000 kwa mwaka.
Kuendelea kutoa elimu ya ugani kwa wavuvi juu ya uvuvi endelevu na wenye tija, kwa wafanyabiashara ya samaki juu ya njia bora na salama za uhifadhi samaki na elimu ya ufugaji samaki ili kuweza kujiongezea kipato na kuinua uchumi.
Kitengo cha uvuvi kinaendelea kufanya doria za mara kwa mara ili kupambana na uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi
Wilaya ya Pangani ni mojawapo ya wilaya zilizochaguliwa kuwa za mfano kutekeleza mradi wa SWIOFish ambapo kitengo cha uvuvi kinatarajia kuimarisha usimamizi wa rasilimali za uvuvi kwa kushirikisha jamii katika kulinda, kutunza, kuhifadhi rasilimali za bahari pia kusimamia sera, sheria na kanuni za uvuvi ili kuwa na uvuvi endelevu kwa manufaa ya jamii na wilaya kwa ujumla.
Kitengo cha uvuvi kinatarajia kutekeleza vipengele vyote vya mradi kikishirikiana na jamii ya wavuvi ili kudumisha usimamizi unaozingatia ekolojia ya mazingia.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa