SEKTA YA MIFUGO
Wilaya ina mifumo mikubwa miwili ya ufugaji wa ng’ombe ikiwemo ufugaji wa kienyeji wa kuchunga na ufugaji wa ndani. Kumekuwepo na ongezeko kubwa la mifugo ya wafugaji wahamaji ambapo kwa sasa kuna jumla yang’ombe 51,303 (46,229 wa asili na 5074 wa kisasa); mbuzi 26,102; kondoo 11947, punda 446 na kuku 110,329. Hali hii ya kuongezeka kwa idadi kubwa ya mifugo imepelekea kuongezeka kwa uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa migogoro ya wakulima na wafugaji.
Uzalishaji wa Maziwa:
Wastani wa jumla ya lita 8,743 hukusanywa kwa siku kwenye vituo vya kukusanyia maziwa vilivyopo chini ya Ushirika wa wafugaji (WAWAPA) na kusafirishwa kwenda Tanga Fresh. Kuna jumla ya vituo 4 vya kukusanyia maziwa katika Wilaya. Jumla ya lita 2,227,035 za maziwa zilikusanywa katika kipindi cha 2015/16.Aidha bei anayopata mfugaji ni TShs. 680/= kwa lita katika vituo.
SEKTA YA UVUVI
UTANGULIZI
Wilaya iinatekeleza shughuli zote za Uvuvi kama ilivyo ada, shughuli hizo ni pamoja na kusimsmia sheria, kanuni na sera za uvuvi ili kuhakikisha kunakuwepo na ulinzi,uhifadhi,utunzaji na uvunaji endelevuwa rasilimali za uvuvi pamoja na utunzaji wa mazingira yake,lengo kuu ni kuhakikisha rasilimali ya uvuvi inatumiwa na kizazi cha sasa na cha baadae kwa maendeleo ya jamii na wilaya kwa ujumla.
HALI YA UVUVI
Hali ya uvuvi katika wilaya yetu ya pangani ni ya wastani pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo za uvuvi haramu zana duni na vyombo duni kwa wavuvi wengi wa pangani lakini shughuli za uvuvi zimeendelea kufanyika hadi kufikia robo ya pili ya mwaka2016/2017 jumla ya kilo 38,525 zenye thamani ya tshs 154,100,000/= zilivunwa.
IDADI YA WAVUVI NA VYOMBO
Kwa mujibu wa sense ya uvuvi iliyofanyika mwezi wa pili mwaka 2016 Wilaya ya Pangani ina jumla ya wavuvi1540 wanaojishughulisha na uvuvi wa samaki, pweza kamba na kaa na wavuvi 62 wanaojighulisha na utandaji wa uduvi ambao kwa mujibu wa sheria ya uvuvi no.22 ya mwaka 2003.
MAFANIKIO
Kitengo cha uvuvi kwa kushirikiana na mamlaka ya chuo cha ufundi stadi VETA kwa awamu tofauti tulifanikiwa kutoa elimu kwa wavuvi sitini (60) juu ya ujasiriamali, uchakataji na usindikaji wa samaki, VVU na Ukimwi kwa wadau wa uvuvi wa vijiji vya Ushongo, Stahabu, Pangani mashariki na Pangani magharibi na (wavuvi kumi na tano kwa kila kijiji) kuweza kutunukiwa vyeti kwa wavuvi hao
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa