IDARA YA UJENZI
Idara ya ujenzi ni mojawapo ya idara kuu zinazounda Halmashauri ya Wilaya ya Pangani. Idara ya Ujenzi ni Idara iliyoundwa katika mamlaka ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI)kwa madhumuni ya Kusimamia na kutengeneza barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Kusimamia Ujenzi wa majengo ya Serikali na kutoa ushauri wa namna iliyobora ya ujenzi huo;
Pia miradi ya Mashirika yasiyo yaki – Serikali pamoja na kutoa ushauri wa ujenzi wa nyumba bora kwa wananchi , Kusimamia matengenezo ya magari, mitambo na nishati ya umeme kwenye majengo ya Serikali katika Halmashauri ya Wilaya.
Idara ya Ujenzi husimamia ukarabati naujenzi wa majengo mbalimbali katika Halmashauri yaWilaya ya Pangani kama ifuatavyo:
Pia idara hutoa ushauri wa namna iliyobora ya ujenzi wa majengo katika miradi ya Mashirika yasiyo ya ki – Serikali pamoja na kutoa ushauri wa ujenzi wa nyumba bora kwa wananchi.
UMEME
Idara ya ujenzi pia kuna kitengo cha umeme. Kitengo hiki kupitia mtaalamu wetu wa idara hufanya shughuli za ukarabati nauwekaji wa mfumo wa Umeme katika majengo yote ya Halmashauri na serikali yaliyopo hapa wilayani.
MAGARI NA MITAMBO.
Idara ya Ujenzi huyafanyia matengenezo madogomadogo magari na mitambo ya serikali katika karakana yake iliyopo ujenzi, pia huratibu na kukagua magari yote ya Halmashauri kwaajili ya matengenezo mbalimbali kupitia mtaalamu wa magari wa Idara. Magari yote ya Halmashauri hukaguliwa kwanza na mtaalamu wa magari wa idara kabla ya kupelekwa kwa wazabuni kwaajili ya matengenezo makubwa
HalmashauriyaWilayaya Pangani kupitia Idara ya ujenzi huzifanyia matengenezo barabara za Halmashauri na vijiji kwa kutumia fedha za mfuko wa barabara kama ifuatavyo:-
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa