Maafisa Habari wa Mkoa, Halmashauri na Taasisi za Umma zilizopo mkoani Tanga ni miongoni mwa wanataaluma hiyo takribani 800 wanaojumuika jijini Dar es Salaam kushiriki Kikao Kazi cha Kitaifa cha Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais kilichoanza tarehe 17 Disemba 2025 na kitafikia kilele chake Disemba 18, 2025.

Kikao hicho kilichofunguliwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt.Moses Kusiluka, kinahudhuriwa pia na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Bakari Machumu, Mshauri wa Rais wa Habari na Mawasiliano, Tido Mhando, miongoni mwa viongozi wengine kadhaa.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa