Waandaaji wa maudhui mtandaoni Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo tarehe 05 Februari 2026 wamejitokeza kuchukua fomu za usajili ili waweze kutambulika na kupata fursa za mikopo zilizotangazwa na Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda.

Zoezi la uandikishaji wa walengwa limeanza Januari 30, 2026 na litakamilika Februari 15, 2026, ambapo watengenezaji wa maudhui wanatakiwa kufika katika ofisi ya Halmashauri kupitia Kitengo cha Mawasiliano ya Serikalini, ili kuchukua na kujaza fomu za maombi, zikiainisha taarifa binafsi pamoja na shughuli wanazozifanya.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa