KITENGO CHA SHERIA
UTANGULIZI.
Kitengo cha sheria ni miongoni mwa vitengo vinavyounda Idara navitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani. Majukumu ya Kitengo chaSheria ni kama yafuatayo:
1. Kutoa ushauri kwa Halmashauri ili kufikiamaamuzi mazuri ambayo humaliza migogoro.
2. Kutunga sheria ndogo za Halmashauri
3. Kuandaa miswada ya sheria ndogo za vijiji kulingana na mahitaji ya Halmashauri au kufuatana na maelekezo tunayopokea.
4. Kuhudhuria kesi mbalimbali Mahakamanizinazoihusu Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri za vijiji na kutoautetezi kwa mujibu wa sheria (Legal AdvocacyDefence)
5. Kutoa taarifa mbali mbali za migogoro yakisheria inayoihusu Halmashauri.
6. Kusaidia Kutatua migogoro mbalimbaliinayowakabili wananchi vijijini baina ya wao wenyewe au serikali za vijiji kwamujibu wa sheria za Nchi.
7. Kuhimiza na kusimamia utawala wa sheria ndani yaHalmashauri na katika serikali za vijiji ili kuhakikisha kuwa haki inatendekana migogoro kumalizika.
8. Kufuatilia misuada, waraka au marekebisho yasheria zinazohusu maslahi ya Halmashauri na kutoa taarifa kwenye Halmashauri kwa wakati.
9. Kufanya upekuzi wa mikataba mblimbali yamanunuzi katika Halmashauri.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa