Kamati ya Elimu na Afya Pangani imetoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule wanaandikishwa kwenye shule za msingi na sekondari ndani ya wilaya hiyo.

Hayo yamefanyika leo tarehe 8 Januari 2026, wakati wa kikao cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri Mkoma.

kamati imeeleza kuwa bado kuna idadi ya watoto ambao hawajaandikishwa licha ya kuwa na umri unaostahili, jambo linaloweza kuathiri malengo ya wilaya katika kuinua kiwango cha elimu na ustawi wa jamii.

Vilevile, kamati imesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wazazi, viongozi wa Vijiji na walimu katika kutoa elimu kuhusu madhara ya kutompeleka mtoto shule, pamoja na kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo mara kwa mara.
Aidha, kamati imehimiza wananchi kutumia kipindi cha uandikishaji kinachoendelea na kusisitiza kuwa serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya shule na huduma za afya ili kuwezesha mazingira bora ya kujifunzia.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa