MAJUKUMU YA JUMLA
- kuweka mikakati na kupendekeza uongezaji wa mapato
- Kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango wa maendeleo kwenye Halmshauri ili kuidhinishwa na Halmashauri
- Kusimamia utunzaji wa hesabu za fedha ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mali za Halmshauri,ukusnyaji wa Mapato,kufuta madeni,na kuomba vibali maalumu kwa matumizi yanayohitaji kibali cha waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa
- Kufukiria na ,pale inapowezekana ,kupendekeza kwenye Halmashauri masuala yanayohusu sharia ndogo na utendaji katika ngazi za chini za Halmashauri
- Kupokea na kuzingatia mapendekezo ya kubadili matumizi ya mafungu ya fedha (re-allocation) yaliyopo katika makisio yalioidhinishwa na kuyapeleka kwa Halmashauri
- Kuratibu mapendekezo kutoka kwenye kamati zingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi nakuyawasilisha kwenye Halmashauri
- Kufikiria na kupendekeza kwenye Halmshauri mikopo yote hya Halamshauri
- Kutoa mapendekezo ya vitega uchumi kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa mujibu ya sharia ya fedha za serikali ya mitaa,sura ya 290
- Kupokea na kujadili taarifa za wakaguzi wa fedha na mali ya Halmshauri na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na maelekezo na maoni ya wakaguzi kwa mujibu wa sharia za serikali za mitaa,sura ya 290
- Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za Halmshauri ,kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na waziri na taratibu nyingine zitakaowekwa na Halmashauri
- Kupitia marekebisho yote yaliyopendekezwa hususani kuhusu taratibu za fedha,ikiwa ni pamoja na mapitio ya mara kwa mara yanayohusu thamani ya fedha ambapo kanuni mbalimbali za manunuzi ya na mali na vifa hutumika;
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa