Pangani DC imeibuka na ushindi muhimu wa goli 1–0 dhidi ya Songea MC katika mchezo wao wa tano wa mashindano ya SHIMISEMITA 2025, uliochezwa leo, 23 Agosti 2025, kwenye Uwanja wa Galanosi, Jijini Tanga.
Bao pekee na la ushindi lilifungwa na Hassan Nindi katika dakika za mwisho za kipindi cha pili, likiiwezesha Pangani DC kupata alama tatu muhimu na kujiimarisha zaidi kwenye mbio za kusaka nafasi ya juu katika kundi lao.
Ushindi huu unaongeza morali ya wachezaji na benchi la ufundi, huku mashabiki wa Pangani DC wakipewa matumaini mapya kuelekea michezo inayofuata ya SHIMISEMITA.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa