Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani,leo tarehe 1 Disemba 2025, wakazi wa Kata ya Kimang’a Wilayani Pangani wamejitokeza kupata elimu na huduma za upimaji wa VVU

Lengo ni kuongeza uelewa kuhusu kinga, kupunguza unyanyapaa, na kuhamasisha wananchi kujua hali zao kwa wakati.

Akiongea katika Maadhimisho hayo Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bi Sophia Kabome amesema kuwa kupima ni hatua muhimu katika kujilinda na kulinda jamii dhidi ya maambukizi mapya.
" Sisi wana Pangani tukiweka nguvu za pamoja tutaweza kutokemeza janga hili na Wilaya yetu inaendelea kupambana na gonjwa hili katika jamii zetu". Alisema.

Kauli mbiu " Shinda vikwazo, imarisha mwitikio tokomeza UKIMWI"
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa