Ujenzi wa madarasa 3 kupitia mradi wa BOOST katika Shule ya Msingi Masaika, wilayani Pangani, unaendelea vizuri.

Hatua kubwa za ujenzi zimekamilika na kazi zinaendelea kwa kasi ili kuhakikisha madarasa yanakamilika kwa wakati uliopangwa.
Mradi huu unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia, kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuongeza ufanisi wa ufundishaji.

Hata hivyo Serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu inaendelea kusimamia mradi huu ili kuhakikisha unakidhi viwango na kutoa matokeo chanya kwa jamii.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa