HUDUMA ZA JAMII SEKTA YA VIJANA.
Kwa kipindi cha robo ya pili (Oktoba-Desemba) Halmashauri kwa kushirikiana na mashirika binafsi ambao ni wadau wa maendeleo ya vijana Wilaya ilifanikiwa kuwapatia vijana mafunzo ya kama vile Kuwawezesha vijana katika ufuatiliaji wa rasirimali za umma katika sekta ya elimu,Kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa vijana.Jumla ya vijana 60 kwa nyakati tofauti waliweza kufaidika katika mafunzo hayo.Kwa kipindi hiki Halmashauri ilishirikinana na wadau wa maendeleo kama vile New Age Foundation(NAF) na Marie Stopes Tanzania.
MFUKO WA VIJANA
Kwa kipindi tajwa mfuko unaendelea vizuri na umefanikiwa kutoa kiasi cha Tsh 2,000,000/= kwa kikundi kimoja cha vijana kinachojishughulisha na ufugaji wa kuku.USHONGO CHICKEN PROJECT. Kwa ongezeko hili limepelekea Mfuko kuweza kuongeza kiwango cha mikopo kwa vijana na kufikia Tsh 39,500,000 kutoka Tsh 37,500,000 kwa ujumla. Mfuko bado unaendelea kufuatilia marejesho ya fedha za mikopo kutoka kwa vikundi vya vijana kwa fedha kutoka wizarani (Tsh 29, 5000, 000) na halmashauri (Tsh 10,000,000) na pia ufuatiliaji wa kesi ya marejesho ya fedha kutoka SACCOS ya vijana (Tsh 13,000,000) unaendelea na kesi bado iko mahakamani.
ASILIMIA TANO
Kwa mujibu ya bajeti ya 2016/2017 halmashauri ilitenga jumla ya Tsh 47,310,500 kama 5% ya mfuko wa maendeleo ya vijana. Jumla ya mapato ya halmashauri kwa nusu mwaka ni Tsh 201,806,359 na kwa kipindi cha robo ya pili imetolewa Tsh 2,000,000 na bado rimbikizo la Tsh 8,090,317.95 kulingana ma mapato halisi.Jitihada za utengaji wa 5% kulingana na bajeti husika na ukusanyaji wa mapato halisi unaendelea.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa