SEKTA YA KILIMO:
80% ya wakazi wa Wilaya ya Pangani ni wakulima na wafugaji wadogowadogo na 20% ya wananchi waliobaki ni wavuvi, wafanyabiashara, wajasiriamali na wafanyakazi
MATUMIZI YA ARDHI
Shughuli za kilimo na ufugaji katika Wilaya ya Pangani zimechukua Hekta 63,876.75. ikiwa Hekta 25,800 hutumiwa na wakulima wadogowadogo, hekta 14,286.75 zinatumika na wakulima wakubwa wa mashamba ya mkonge, Hekta 23,790 zinatumika kwa malisho kati ya Hekta 122,500 zinazofaa kwa kilimo
MAFANIKIO YA SEKTA YA KILIMO
Wakulima wa korosho Kijiji cha Sange wamenunuliwa mashine za ubanguaji korosho.
Vikundi 7 vya uzalishaji miche ya korosho vimeanzishwa na hadi 2016/17 jumla ya miche bora ya Mikorosho 120,000 na itagawiwa bure kwa wakulima.
• Ushirika wa wakulima wa nazi wamenunua mashine za kuchakata makumbi ya nazi hivyo kuongeza thamani ya zao la minazi
SEKTA YA USHIRIKA:
Wilaya ya Pangani ina jumla ya vyama vya Ushirika 30 vilivyoandikishwa, vikiwemo 5 vya mazao, 22 vya Ushirika wa Kuweka na Kukopa, 2 vya maziwa na 1 cha wavuvi. Aidha kuna vyama 2 vya mazao (AMCOS) ambavyo vimeshaundwa na maombi ya usajili yametumwa kwa msajili wa vyama kwa ajili ya kukamilisha uundaji wa chama. Vyama vyote vya Ushirika vina jumla ya wanachama 2,454 wa vyama mbalimbali vya Ushirika wakiwemo wanaume 1,560 na wanawake 857 na vikundi 37.
Kuna jumla ya SACCOS 22 zenye jumla ya wanachama 2,102. Thamani ya mafungu ni 10,400 yenye thamani 103,410,400, akiba ya TShs. 214,662,111.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa