Taasisi isiyo ya Kiserikali ya CAMFED imeendelea na mafunzo kwa wajumbe wapya wa Kamati ya CDC Wilayani Pangani kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya elimu.
Mafunzo hayo yalifunguliwa tarehe 19 Agosti 2025 katika ukumbi wa TRC na Afisa Elimu Sekondari, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CDC, Bi. Lucy Gurtu, aliyepongeza CAMFED kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kwa vitendo.
Mwezeshaji kutoka CAMFED, Mwalimu Noel Stephen Kombo, alisema mafunzo hayo ni muhimu kwani wajumbe wa CDC ndio kiungo muhimu cha kuunganisha jamii na kuhakikisha miradi ya elimu inaleta matokeo chanya. Aidha, aliwasilisha mada mbalimbali ikiwemo majukumu ya CDC, taratibu za utoaji wa fedha na umuhimu wa kuzingatia kanuni na miongozo iliyopo.
Kwa upande wake, mwezeshaji mwingine kutoka CAMFED, Ndugu Deogratias Mbwani, aliwasilisha mada kuhusu manunuzi, akibainisha hatua muhimu zinazopaswa kuzingatiwa na kueleza kuwa CDC ina jukumu kubwa la kusimamia manunuzi mbalimbali kwa kufuata taratibu sahihi.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 21 Ag
osti 2025.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa