MAZINGIRA
Wilaya inatekeleza kampeni ya usafi wa mazingira ikiongozwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ikishirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi. Kupitia kampeni hii, wananchi pamoja na viongozi wa serikali za vijiji na watendaji hushiriki kikamilifu katika zoezi hili na limeleta mafanikio kwa kupunguza uchafu katika maeneo mengi ya mjini na vijijini. Aidha wilaya inasimamia usafi wa fukwe katika vijiji vilivyoko pembezoni mwa Bahari ya Hindi ili kuwa kivutio kwa watalii wanaofika kutembelea maeneo hayo.
Ili kuhakikisha kwamba fukwe zinakuwa safi muda wote, kamati za usimamizi wa mazingira ya Pwani (BMU) zimepatiwa mafunzo ya kufanya doria, kulinda na kuendeleza hifadhi na maliasili zilizopo katika maeneo hayo. Aidha, kamati hizi zimepatiwa vifaa vya usafi kutoka kwa wafadhili mbalimbali.
Katika kuhakikisha kwamba jamii inashiriki kikamilifu katika zoezi la usafi wa mazingira, elimu imeendelea kutolewa kupitia wadau mbalimbali kama vile; Asasi ya kuhifadhi Kasa (SEA SENSE) pamoja na Radio jamii (Pangani Fm radio) ambapo kuna kipindi maalum cha mazingira kinachorushwa kila siku ya Jumanne. Radio hii husikika katika maeneo yote wilayani na wilaya za jirani.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa