1; JIOGRAFIA YA WILAYA
Wilaya ya Pangani ni miongoni mwa wilaya nane (8) na Halmashauri kumi na moja (11) zinazounda Mkoa wa Tanga. Kijiografia Wilaya ya Pangani iko kusini mwa Jiji la Tanga, kwa upande wa Mashariki inapakana na Bahari ya Hindi, Magharibi Wilaya ya Handeni, Kaskazini Wilaya ya Muheza na Kusini Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Wilaya ipo Kms 47 kutoka Makao Makuu ya Mkoa. Wilaya ina ukubwa wa eneo la Kilomita za Mraba (KM 2) 1,830.8, na sehemu kubwa iko kwenye ukanda wa Pwani ambapo mto Pangani unaingia Bahari ya Hindi.
1.2: UTAWALA NA IDADI YA WATU
Wilaya ya Pangani inaundwa na Tarafa 4, Kata 14, Vijiji 33 na vitongoji 96. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ilikuwa na jumla ya watu 54,025 kati ya hao wanaume walikuwa ni 26,870 na wanawake 27,155 na kaya zilikuwa 13,177 Kwa sasa wilaya inakadiriwa kuwa na watu 59,502 wakiwemo wanaume 29,571 na wanawake 29,931, zipo kaya 14,413 zenye ukubwa wa wastani watu 4.1 kwa kaya. Ongezeko la watu kwa mwaka linakadiriwa kuwa ni 2.2% na msongamano wa watu kwa Kilomita moja ya Mraba (1Km2) ni watu 29.5.
Jedwali 1: Muundo wa Wilaya Kiutawala
TARAFA
IDADI YA KATA
IDADI YA VIJIJI
IDADI YA VITONGOJI
MADANGA4
9
32
PANGANI3
3
10
MWERA5
15
39
MKWAJA2
6
15
Jumla14
33
96
2. HALI YA HEWA
Wilaya ipo kwenye ukanda wa pwani, katika mwinuko kati ya mita 0 – 100 kutoka usawa wa bahari. Wilaya hupata mvua za Vuli, Masika na mchoo zenye wastani wa kati ya mm 1000 – 1500 kwa mwaka.
VULI – (Oktoba- Disemba) Wastani ni Mm 500- Mm 800
MASIKA – (Machi- Mei) Wastani ni Mm 1000- Mm 1400
MCHOO – (Julai- Agosti) Wastani ni Mm 100
3.0: HALI YA ULINZI NA USALAMA
Hali ya usalama katika Wilaya kwa ujumla ni shwari na tulivu. Hakuna matukio makubwa ya kihalifu yaliyojitokeza kwa kipindi kirefu sasa hali ni shwari. Katika kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao wilaya imekuwa ikiendelea kutoa mafunzo ya Mgambo kila mwaka pamoja na mafunzo ya polisi jamii. Tunawashukuru wananchi kwa ushirikiano wanaotupatia. Aidha kwa kutumia vyombo vya Dola, Wilaya inaendelea kudhibiti makosa ya kawaida, Jinai, madai na usalama barabarani kwa mujibu wa sheria
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa