Mamlaka ya Maji Mjini inahudumia Mji wa Pangani pamoja na Vijiji vinavyouzunguka Mji huu. Jumla ya wakazi wapatao 14,423 walilengwa kupata kupata huduma ya Maji safi kutoka katika Visima Virefu (BH) 4 vilivyoko katika Kijiji cha Boza. Hata hivyo, idadi ya watu wanaopata Maji ni 8,076 ambao ni sawa na asilimia 56 (56%) ya walengwa wote.
Lakini kutokana na kuharibika mara kwa mara kwa mitambo chakavu ya kusukuma maji, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa muda mwingi inakadiriwa kuwa chini ya asilimia 45 ya mahitaji .
Pamoja na matatizo mengine, Mradi wa Maji Mjini unakabiliwa na changamoto kuu zifuatazo;
a)Tofauti kubwa iliopo baina ya utashi na ugavi
(Demand and Supply), uzalishaji wa Maji ni mita za ujazo 900 kwa siku wakati mahitaji ya Maji ni mita za ujazo 1,600 kwa siku sawa na asilimia 56 (56%).
b) Miundombinu ya kusambaza Maji na Mitambo chakavu; Miundombinu ya kusambaza Maji imejengwa kwenye miaka ya 1960s na kwa sasa imechakaa sana na huathiri utoaji wa huduma kwa kiasi kikubwa
c) Katizo la umeme la mara kwa mara; kutokana na kutokuwepo kwa ‘’standby Generator’’, kiwango cha uzalishaji Maji hupungua sana.
d) Kiwango kikubwa cha upotevu wa maji (non revenue water) kutokana na wateja wengi kutokuwa na dira za maji.
Ili kukabiliana na changamoto zilizoainishwa hapo juu, Wizara ya Maji ilimwajiri Mtaalamu Mshauri (ARAB CONSULTING ENGINEERS) kufanya upembuzi yakinifu ( Feasibility studies) mwaka 2009.
Mtaalamu Mshauri alitoa mapendekezo yafuatayo:-
a) Ufumbuzi wa muda mfupi (Short term solution) kuongeza uzalishaji Maji kwa kuchimba Visima virefu 3 na kuboresha Miundombinu ya kusambaza Maji kwa makadirio ya gharama Tsh. 747,000,000/= (2009).
b) Ufumbuzi wa muda mrefu (Long term solution) unalenga kuchukua maji kutoka mto Pangani na makadirio ya gharama za utekelezaji ni Tsh Bilioni.10.6 (2009).
UKARABATI WA MRADI WA MAJI MJINI.
Kupitia maombi maalum (Other Grants) 2014/2015 Halmashauri ya Wilaya ilipokea kiasi cha Tsh 200,000,000 kati ya Tsh 400,000,000 zilizoombwa kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya mradi wa maji Mjini awamu ya kwanza. Kwa sasa ukarabati wa miundombinu ya usambazaji maji awamu ya kwanza umekamilika. Hatua hii imesaidia kuongeza kiwango cha uzalishaji wa Maji na kuwa mita za ujazo 900 kwa siku kutoka mita za ujazo 700 kwa siku.
Katika bajeti ya mwaka 2015/16, kwa upande wa maji mjini tuliidhinishiwa Tshs 200 milioni kupitia maombi maalum (Other Grants) lakini hatukupokea fedha hizo.
Mwezi Oktoba 2016 tumepokea Tshs 200 milioni kutoka Wizara ya maji kwa ajili ya kuendeleza ukarabati wa miundo mbinu ya kusambaza maji mjini awamu ya II na kuweka mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji mapato . Hata hivyo ni muhimu kwa fedha kuendelea kupatikana ili ukarabati uweze kufanyika awamu kwa awamu.
MAJI VIJIJINI
Malengo ni kuona kuwa upatikanaji wa maji katika umbali usiozidi mita 400 kutoka makazi ya wananchi. Kupitia Programu ya Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (NRWSSP), Ujenzi wa miradi ya Maji katika vijiji nane vya Madanga, Jaira, Bweni, Kwakibuyu, Kigurusimba, Mzambarauni, Boza na Madanga imekamilika.
Wakazi wa Vijijini wapatao 29,560 hupata huduma ya maji safi karibu na makazi yao ambapo ni sawa na 66% ya wakazi wote 44,788 wa Vijijini.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa