Wakazi zaidi ya 3,500 Mkwaja kunufaika na maboresho ya huduma za afya

Wakazi zaidi ya 3,500 wa kata ya Mkwaja wilayani Pangani wanatarajiwa kunufaika na maboresho ya huduma za afya baada ya Serikali kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo matundu matatu ya vyoo vya wagonjwa, kichomea taka, mnara pamoja na maeneo ya kunawia mikono katika kituo cha afya cha eneo hilo.

Maboresho hayo yamebainishwa leo, tarehe 7 Januari 2026, wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Ndg. Agape Fue.

Amesema ujenzi wa miundombinu hiyo unalenga kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya, kuongeza usafi na usalama katika utunzaji wa taka za hospitali, pamoja na kupunguza maambukizi yatokanayo na uchafu katika maeneo ya kutolea huduma.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kulinda na kutunza miundombinu hiyo ili iendelee kuwanufaisha kwa muda mrefu.

Wananchi wa Mkwaja wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo, wakisema maboresho hayo yatasaidia kuongeza ufanisi wa huduma za afya na kupunguza changamoto walizokuwa wakizipata hapo awali.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa